Maelfu ya wafungwa kote nchini Nigeria wameachiliwa kutoka gerezani katika juhudi za kukabiliana na msongamano wa watu, waziri wa mambo ya ndani Olubunmi Tunji-Ojo alisema Jumamosi kwenye mtandao wa kijamii.
Hatua hiyo ni sehemu ya harakati za Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu, ambaye alichaguliwa mapema mwaka huu, kupunguza msongamano katika magereza ya Nigeria yenye idadi kubwa ya watu.
Jana, tulitangaza kuachiliwa kwa wafungwa 4,068 kati ya 80,804 katika jela zetu 253 kote nchini kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kulipa faini, Olubunmi Tunji-Ojo aliandika katika taarifa yake kwenye mtandao wa X.
Alitoa tangazo hilo baada ya kuitembelea jela ya Kuje karibu na mji mkuu Abuja.
Forum