Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:44

Rais mpya wa Liberia atangaza vita vya kitaifa dhidi ya dawa za kulevya


Rais mpya wa Liberia Joseph Boakai akiwa kwenye makao yake mjini Monrovia
Rais mpya wa Liberia Joseph Boakai akiwa kwenye makao yake mjini Monrovia

Rais mpya wa Liberia Joseph Boakai ametangaza utumizi wa dawa za kulevya kuwa dharura ya afya ya umma, huku akiteuwa kamati maalum ya kushugulikia tatizo hilo, wakati alipokuwa akitoa hotuba ya kwanza kwa taifa Jumatatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, dawa ya kulevya aina ya Kush, inayotengenezewa viwandani, na yenye athari sawa na bangi, imeshamiri zaidi miongoni mwa vijana nchini Liberia, pamoja na jirani wake Sierra Leone.

Ni rahisi kutambua watumizi wake kutokana na ulevi wa aina yake, wakati wakionekana kwenye mitaa ya mabanda pamoja na ile ya kifahari. Boakai wakati wa hotuba yake ya dakika 40 mbele ya bunge, alisema kwamba yeye na naibu wake watakuwa wa kwanza kufanyiwa vipimo vya dawa, tangazo lililokaribishwa kwa furaha na wabunge.

“Utumizi wa dawa za kulevya na hasa Kush nchini mwetu, ni tishio kubwa kwa watoto wetu pamoja na taifa kwa ujumla,” aliongeza Boakai. Rais wa zamani George Weah aliyeshindwa na Boakai kwenye uchaguzi wa Novemba, wakati wa kampeni alikosolewa pakubwa kwamba alishindwa kukabiliana na tatizo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG