Mamlaka imekiri kulikuwa na matatizo lakini wakatupilia mbali madai kuwa kura ziliibiwa. Mzozo huo uliozua tafrani unarudia mizozo ya awali ya uchaguzi ambayo ilichochea machafuko nchini Congo.
Tshisekedi alikula kiapo kwenye uwanja wa michezo katika mji mkuu Kinshasa uliokuwa umejaa wafuasi wakipeperusha bendera ndogo ndogo, maafisa wa serikali, wakuu wa nchi za Afrika na wajumbe wengine wa kigeni wakiwemo kutoka Marekani, China na Ufaransa.
Huku askari walio na silaha wakiwa wametapakaa kote katika mji mkuu, kulikuwa hakuna ishara ya mara moja kwamba wafuasi wa upinzani mjini Kinshasa walikuwa wakisikiliza wito kutoka kwa wapinzani wawili wakuu wa Tshisekedi kupinga kuchaguliwa kwake tena.
Forum