Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak wamekubaliana kuimarisha uhusiano wa karibu wa kiuchumi kati ya nchi zao, na kuahidi kuharakisha kipindi cha kuanza kutumia nishati safi na kuimarisha njia za usafiri wa madini nyeti.
Viongozi hao wawili pia walijadili uungaji mkono wao usioyumba kwa watu wa Ukraine, Biden aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja akiwa na Sunak, fursa ambayo haitolewi kwa kila kiongozi wa dunia anayetembelea White House.
Biden na waziri mkuu wa Uingereza walitoa Tangazo la Atlantic ambalo Sunak alilielezea kama ushirikiano wa kwanza wa kiuchumi wa aina yake juu ya masuala kama teknolojia mpya ya program ya computer AI, mabadiliko ya hali ya hewa, na kulinda teknolojia ambazo zitasaidia kuunda mfumo bora zaidi siku zijazo.
Rais Biden alisifu kuimarika haraka ushirikiano wa kiuchumi kua ni chanzo cha nguvu ambacho kinamulika uhusiano mpana kati ya washirika wa NATO. Tulijadili jinsi tunavyoweza kuendelea kukabiliana na kuboresha ushirikiano wetu ili kuhakikisha nchi zetu ziko mbele katika teknolojia mpya inayobadilika haraka duniani, alisema.
Forum