Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 09:31

Rais Biden anajiandaa kwa kampeni akipigia debe ajenda yake ya "Bidenomics"


Rais wa Marekani, Joe Biden
Rais wa Marekani, Joe Biden

Rais Biden anapigia debe ajenda ya Bidenomics akilinganisha maoni yake ya kujenga uchumi kutoka chini hadi katikati na kile kinachoitwa MAGA Republicans

Rais wa Marekani Joe Biden akijiandaa kwa ajili ya kampeni yake ya kuchaguliwa tena mwaka 2024, siku ya Jumatano aliipigia debe ajenda yake ya “Bidenomics”, akilinganisha maono yake ya kujenga uchumi “kutoka chini hadi kati-kati”, na kile kinachoitwa MAGA Republicans ambao wanaunga mkono ajenda ya Rais wa zamani Donald Trump ya Make America Great Again.

Biden alitetea vipengele vya sheria vya utawala wake dhidi ya mashambulizi yao, ikijumuisha sheria yake ya hali ya hewa na nishati mwaka 2022 inayojulikana kama Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei, na Sheria yake ya Miundombinu ya pande zote mbili za vyama ya 2021, pamoja na Sheria ya Huduma ya Afya ya bei nafuu ya enzi ya Obama ambayo iliongeza fursa ya upatikanaji wa bima ya afya.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson, Donald Trump na Warepublican wa MAGA katika Bunge, wamejitolea kulinda kukatwa kwa kodi kwa watu wenye kipato cha juu sana. Na wataendelea kupinga kuwekeza katika programu zote ambazo zinawasaidia watu, iwe katika elimu, huduma za afya, au chochote, Biden alisema katika hotuba yake katika CS Wind, mtengenezaji mkubwa zaidi wa mnara wa upepo duniani, huko Pueblo, katika jimbo la Colorado.

Forum

XS
SM
MD
LG