Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 18:25

Raia wa Russia ahukumiwa miaka saba jela kwa kupinga vita vya Ukraine


Artyom Kamardin aliyesimama (C) wakati akisomewa hukumu katika mahakama huko Moscow hapo Desemba 28, 2023.
Artyom Kamardin aliyesimama (C) wakati akisomewa hukumu katika mahakama huko Moscow hapo Desemba 28, 2023.

Artyom Kamardin alikutwa na mashtaka ya kusoma mashairi yanayopinga vita wakati wa maonyesho ya mtaani mjini Moscow Septemba 2022.

Mtunzi wa mashairi raia wa Russia alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela siku ya Alhamisi, kwa kukariri mistari dhidi ya vita vya Russia nchini Ukraine, adhabu kali ambayo inakuja wakati wa ukandamizaji usiosita wa Kremlin dhidi ya upinzani.

Mahakama ya Wilaya ya Tverskoi ya Moscow ilimhukumu Artyom Kamardin kwa mashtaka ya kutoa wito wa kudhoofisha usalama wa taifa na kuchochea chuki, ambayo ilihusiana na yeye kusoma mashairi yake ya kupinga vita wakati wa maonyesho ya mtaani mjini Moscow hapo Septemba 2022.

Yegor Shtovba, ambaye alishiriki katika tukio hilo na kukariri mistari ya Kamardin, alihukumiwa miaka mitano na nusu kwa mashtaka hayo-hayo. Mkutano huo karibu na mnara wa muimba mashairi Vladimir Mayakovsky ulifanyika siku chache baada ya Rais Vladimir Putin kuamuru uhamasishaji wa wanajeshi wa akiba 300,000 wakati jeshi la Moscow likipata bahati mbaya huko nchini Ukraine.

Hatua hiyo ambayo haikupendwa sana ilichochea maelfu kuikimbia Russia ili kuepuka kuandikishwa katika jeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG