“Siku zote tumekuwa tukisema tuko tayari kwa mazungumzo na maelewano,” Putin aliwaambia waandishi wa habari, baada ya kusema kwamba vikosi vya Russia, vinasonga mbele kuelekea kufikia malengo yake makuu nchini Ukraine.
Pia amesema yuko tayari kukutana na Trump. “Hivi karibuni, wale Waukraine wanaotaka kupigana watakwisha, kwa maoni yangu, muda si mrefu hakutakuwa na anayetaka kupigana.
Tuko tayari,” Putin aliongeza kusema kwamba upande mwingine unahitaji kuwa tayari kwa mazungumzo na maelewano.
Mwezi uliopita, ripoti za vyombo vya habari zilisema Putin alikuwa tayari kuzungumzia makubaliano ya kusitisha mapigano na Trump.
Forum