Washabiki wa mpira duniani kote wanasubiri kwa hamu fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Croatia.
Lakini nchini Uganda polisi na washabiki wanaangalia jinsi ya kuimarisha usalama katika maeneo yaliyopanga kuonyesha michuano hiyo.
Bado wananchi wa Uganda wanakumbuka vilivyo shambulizi la 2010 ambalo liliuwa washabiki waliokuwa wanashuhudia fainali ya Kombe la Dunia
Polisi wamewataka wananchi wa Uganda kuwa macho na kuripoti aina yoyote ya hatari wanayoishuhudia.
Uganda inapitia mwaka wa nane tangu mabomu mawili yalipuke kwa pamoja mjini Kampala na kuuwa watu wasiopungua 76 waliokuwa wamekusanyika kuangalia fainali ya Kombe la Dunia. Mamia wengine walijeruhiwa.