Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:38

Polisi kisiwa cha Maui nchini Marekani wametoa orodha ya waliopotea kwa ajali ya moto


Maafa yaliyosababishwa na moto uliozuka kisiwa cha Maui nchini Marekani
Maafa yaliyosababishwa na moto uliozuka kisiwa cha Maui nchini Marekani

Katika taarifa ya video iliyotolewa Alhamisi jioni, Mkuu wa Polisi wa Maui, John Pelletier alisema anaelewa kutolewa kwa orodha hiyo kunaweza kusababisha maumivu kwa wale ambao wapendwa wao bado hawajulikani walipo lakini idara ya polisi inahisi inaweza kusaidia katika uchunguzi

Polisi katika kisiwa cha Hawaii cha Maui nchini Marekani wametoa majina ya watu 388 ambao bado hawajulikani walipo kufuatia moto mkubwa wa msituni uliowaka mapema mwezi huu.

Katika taarifa ya video iliyotolewa Alhamisi jioni, Mkuu wa Polisi wa Maui, John Pelletier alisema anaelewa kutolewa kwa orodha hiyo kunaweza kusababisha maumivu kwa wale ambao wapendwa wao bado hawajulikani walipo lakini idara ya polisi inahisi inaweza kusaidia katika uchunguzi.

Orodha ina majina na maeneo ya mawasiliano kwa kila mtu aliyepotea ambaye ameripotiwa. Pelletier aliomba mtu yeyote ambaye ataliona jina lake kwenye orodha au kuwa na taarifa kuhusu mtu aliyepo kwenye orodha hiyo awasiliane na polisi wa Maui au FBI.

Shirika la habari la Associated Press linaripoti kuwa kufuatia moto wa msituni wa mwaka 2018 huko Paradise, California, maafisa waliweza kupunguza orodha ya watu waliopotea kutoka 1,300 hadi 12 ndani ya mwezi mmoja baada ya kutoa orodha ya wale walioripotiwa kupotea.

Forum

XS
SM
MD
LG