Polisi wanaoshughulika na masuala ya fedha wa Italy walikadiria kwamba kasha hilo ambalo lilikuwa limefungwa kwa plastiki lina thamani ya euro milioni 400 ambazo ni karibu dola milioni 450 za kimarekani, kwa bei ya mtaani.
Wachunguzi wanakisia kwamba mzigo huo uliachwa baharini na meli ya kubebea mizigo, kwa mpango wa kutumia boti nyingine ndogo kuuleta kwenye nchi kavu. Polisi walitumia ndege karibu na mahala kasha hilo lilipopatikana, ili kuchunguza iwapo kulikuwa na mengine yalioachwa baharini pia.
Kwa ujumla polisi walihesabu zaidi ya paketi 1,600 za cocaine zikiwa zimefungwa kwe vivurushi 70, taarifa imeongeza.