Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:31

Polisi Uturuki wamemkamata mtu mwenye silaha aliyewashikilia mateka


Ramani ya uturuki na nchi zilizo jirani nazo
Ramani ya uturuki na nchi zilizo jirani nazo

Ofisi ya gavana wa Kocaeli imesema kuwa mateka hao waliokolewa salama.

Polisi walimkamata mtu mwenye silaha ambaye aliwashikilia wafanyakazi mateka katika kiwanda cha Procter & Gamble kilichopo kaskazini magharibi mwa Uturuki siku ya Alhamisi na waliwaokoa mateka saba, na kusitisha maandamano dhidi ya kampeni ya kijeshi ya Israeli huko Gaza, Ofisi ya gavana wa eneo hilo imesema.

Ofisi ya gavana wa Kocaeli imesema kuwa mateka hao hawakujeruhiwa, na kuongeza kuwa operesheni ya kuwaokoa ilifanywa baada ya mazungumzo na mtekaji nyara kufeli.

“Vikosi vyetu vya usalama viliingilia kati na kumtelekeza mshukiwa”, taarifa ilisema na kuongeza kuwa mshukiwa alikuwa mfanyakazi wa kiwanda hicho ambapo alitaka kupewa kipaumbele juu ya kile kinachoendelea huko Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG