Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 19:18

Polisi DRC wamezuia maandamano yaliyoitishwa na upinzani nchini humo


Polisi wa DRC wakiwatawanya wafuasi wa kiongozi wa chama cha upinzania Martin Fayulu huko Kinshasa. Disemba 27, 2023.
Polisi wa DRC wakiwatawanya wafuasi wa kiongozi wa chama cha upinzania Martin Fayulu huko Kinshasa. Disemba 27, 2023.

Polisi mjini Kinshasa walizingira makao makuu ya Martin Fayulu, mmoja wa wapinzani watano wa Rais Felix Tshisekedi wa DRC

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumatano wakati polisi wa kutuliza ghasia walipotawanya kwa nguvu maandamano ya upinzani yaliyopigwa marufuku, ambao wanatoa wito wa kufanyika tena kwa uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita.

Upigaji kura wenye mzozo unatishia kuiyumbisha zaidi Kongo ambayo ni maskini, na tayari inakabiliwa na mgogoro wa usalama mashariki ambao umekwamisha maendeleo katika nchi hiyo yenye uzalishaji mkubwa wa madini ya cobalt na madini mengine ya viwandani na shaba.

Martin Fayulu, mmoja wa wapinzani wa Rais Felix Tshisekedi wa DRC
Martin Fayulu, mmoja wa wapinzani wa Rais Felix Tshisekedi wa DRC

Polisi walizingira makao makuu ya Martin Fayulu, mmoja wa wapinzani watano wa Rais Felix Tshisekedi ambao walikuwa wametoa wito kwa wafuasi wao kuandamana mjini Kinshasa siku ya Jumatano, dhidi ya uchaguzi wa rais na wabunge, ambao wanasema ulikuwa wa udanganyifu na unapaswa kufutwa. Utawala wa Tshisekedi umepuuzilia mbali madai hayo.

Tshisekedi “hakushinda uchaguzi, ushindi wake ni wa udanganyifu,” alisema mwandamanaji mmoja, ambaye alitaja jina lake kama Jean-Pierre.

Forum

XS
SM
MD
LG