Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 16:11

Poland inakaribia kumaliza vizuizi vya malori kwenye mpaka na Ukraine


Madereva wa malori wakiwa wameegesha magari yao kwenye mpaka wa Poland na Ukraine, karibu na kijiji cha Korczowa. Nov. 19, 2023.
Madereva wa malori wakiwa wameegesha magari yao kwenye mpaka wa Poland na Ukraine, karibu na kijiji cha Korczowa. Nov. 19, 2023.

Madereva wa Poland wamekuwa wakizuiwa vivuko  kadhaa na Ukraine tangu Novemba 6.

Serikali ya Poland inakaribia kumaliza vizuizi vya malori katika vivuko kadhaa vya mpaka na Ukraine, waziri mkuu alisema Jumatano.

Madereva wa Poland wamekuwa wakizuiwa vivuko kadhaa na Ukraine tangu Novemba 6, wakidai Umoja wa Ulaya urejeshe mfumo ambao makampuni ya Ukraine yanahitaji vibali vya kufanya kazi katika eneo na hivyo-hivyo kwa malori ya Ulaya kuingia Ukraine.

Wakulima walisitisha maandamano katika moja ya kivuko cha mpakani siku ya Jumapili, lakini madereva wa malori wameendelea kuvizuia vingine vitatu. “Tuko karibu na imani kwamba hatua zetu zinaweza kuleta matokeo, kote kwa mazungumzo huko Kyiv na Brussels,” Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

“Sidhani kwamba tutafanikisha kile ambacho madereva wanakitaka, lakini inaonekana kile ambacho kinaweza kufanikiwa kitaturuhusu kupunguza hisia na kupunguza vizuizi kwenye mpaka”. Mfumo wa vibali kwa madereva wa Ukraine uliondolewa baada ya EU na Kyiv kusaini makubaliano hapo Juni 29 mwaka 2022, miezi minne baada ya uvamizi kamili wa Russia nchini Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG