Wafungwa ambao bado wako katika kituo cha Marekani cha Guantanamo Bay nchini Cuba wanaonyesha dalili za kuzeeka kwa haraka kulingana na afisa mwandamizi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Patrick Hamilton ambaye alishtushwa na hali ya kimwili na maisha ya wafungwa hao wakati wa ziara yake ya karibuni.
Nilishangazwa sana na namna wale ambao bado wanashikiliwa hii leo wanavyokabiliwa na dalili za kuzeeka kwa kasi ongezeko la athari za uzoefu wao na miaka waliyokaa kizuizini, Patrick Hamilton, mkuu wa ujumbe wa ICRC kwa Marekani na Canada alisema katika taarifa.
Ziara yake ya mwisho kabla ya ile ya karibuni ilikuwa mwaka 2003. “Kuna haja ya mtizamo wa kina zaidi kama Marekani itaendelea kuwshikilia wafungwa kwa miaka kadhaa ijayo,” Hamilton alisema. Alitoa wito kwa wafungwa kupatiwa fursa ya kutosha kwa huduma za afya ambazo zinachangia kuzorota kwa hali ya afya ya akili na mwili.
Akiongezea kuwa miundombinu ya kituo hicho inapaswa kubadilishwa iendane na mahitaji ya wafungwa na izingatie mahitaji yao na ulemavu. Mtazamo kamili pia unahitajika alisema, ili kuboresha ubora wa mawasiliano ya wafungwa kwa familia zao.