Wakati akihutubia mkutano wa hadhara huko St Peter’s Square mjini Vatican Jumapili, kiongozi huyo amesema kwamba ziara hiyo pia itatoa nafasi ya kukumbatia jamii ya wakatoliki waliopo, akisema kwamba kanisa hilo lina wafuasi wachache nchini Mongolia, lakini ni wachangamfu na wenye moyo wa ukarimu.
Papa Francis ataondoka Italy Alhamisi kwa ziara hiyo itakayochukua siku nne. Mongolia inasemekana kuwa na wakatoliki 1,500, ikiwa miongoni mwa mataifa yenye watu wachache zaidi ulimwenguni, kwa kuwa na jumla ya wakazi milioni 3.2 pekee.
Kiongozi huyo ameongeza kusema kwamba Mongolia ina utajiri mkubwa wa tamaduni za kidini na kwamba atafurahia kuhudhuria tamasha la pamoja la dini tofauti litakalofanyika Septemba 3. Asilimia kubwa ya wakazi wa Mongolia ni wa Budha.
Forum