Papa Francis alituma salamu kwa China siku ya Jumapili, akiwaita raia wake watu wa heshima na kuwataka Wakatoliki nchini China kuwa wakristo wema na raia wema katika ombi lake la hivi karibuni kwa nchi hiyo ya kikomunisti ili kupunguza masharti ya kidini.
Francis alitoa maoni hayo ambayo hayakuwa yameandikwa katika hotuba yake mwishoni mwa Misa katika mji mkuu wa Mongolia, akiwaita maaskofu wakuu wa zamani na wa sasa wa Hong Kong, Kadinali John Tong Hon na Askofu Mkuu Stephen Chow kushikana naye mikono wakati alipokuwa akizungumza.
Maaskofu hawa wawili ndugu askofu mstaafu wa Hong Kong na askofu wa sasa wa Hong Kong. Ningependa kuchukua fursa ya uwepo wao kutuma salamu njema kwa watu mashuhuri wa China alisema kwa Kiitaliano.
Forum