Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 02:21
VOA Direct Packages

Papa Francis atangaza kuwachagua makadinali wapya


Kiongozi wa kanisa Katiliki Papa Francis akipungia mkono waumini mjini Vatican
Kiongozi wa kanisa Katiliki Papa Francis akipungia mkono waumini mjini Vatican

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis Jumapili ametangaza kuwachagua makadinali wapya 21 wakiwemo viongozi wa kidini kutoka Jerusalem na Hong Kong, sehemu  ambako wakatoliki ni wachache.

Papa Francis alitangaza uteuzi wake mbele ya umati mkubw kwenye eneo la St Peter mjini Vatican, akisema kwamba hafla ya kuwasimika rasmi itafanyika Septemba 30.

Miongoni mwa walioteuliwa ni viongozi kadhaa ambao wanashikilia nyadhifa za juu huko Vatican, kama vile askofu mkuu kutoka Argentina Victor Manuel Fernandez ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Papa kuongoza ofisi ili kuhakikisha sheria za kidini zinafuatwa.

Makadinali wengine ni pamoja na Askofu Stephen Sau-yan Chow, kutoka Hong Kong, pamoja na afisa wa ngazi ya juu wa Vatican kutoka eneo la Mashariki ya Kati, Monsignor Pierbattista Pizzaballa, kiongozi wa kidini kutoka Jerusalem.

Forum

XS
SM
MD
LG