Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:54

Ousmane Sonko wa Senegal atafikishwa mahakamani Mei 16


Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani nchini Senegal
Ousmane Sonko, kiongozi wa upinzani nchini Senegal

Spika mwenye nguvu katika siasa aliyeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa rais nchini Senegal mwaka 2019, Sonko amekuwa akifurahia kuongezeka kwa kasi kisiasa kutokana na umaarufu wake na vijana na amejitangaza kuwa mgombea wa uchaguzi wa 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko atafikishwa mahakamani Mei 16 kwa madai ya ubakaji, wakili wa mshtakiwa wake El Hadji Diouf alisema Jumamosi, akithibitisha ripoti kwa vyombo vya habari.

Spika mwenye nguvu katika siasa aliyeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa rais nchini Senegal mwaka 2019, Sonko amekuwa akifurahia kuongezeka kwa kasi kisiasa kutokana na umaarufu wake na vijana na amejitangaza kuwa mgombea wa uchaguzi wa 2024.

Hata hivyo amekuwa na matatizo kadhaa ya kisheria, hata hivyo alituhumiwa kwa kumbaka mfanyakazi wa saluni ya urembo mahala ambako alikwenda kukandwa misuli.

Sonko, ambaye ni mkaguzi wa zamani wa kodi mwenye umri wa miaka 48 amekanusha shutuma hizo na kusema yeye ni muathirika wa njama zilizopangwa na Rais Macky Sall akitaka kuvuruga azma yake ya kuwania urais mwaka 2024.

Kukamatwa kwa Sonko hapo Machi mwaka 2021 kulisababisha siku kadhaa za ghasia mbaya ambapo watu wasiopungua 12 waliuawa.

XS
SM
MD
LG