Rais Barack Obama wa Marekani atatembelea Kenya mwezi Julai mwaka huu kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi duniani kuhusu ujasiriamali, White House imetangaza Jumatatu.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rais Obama kutembelea Kenya, ambako ni nyumbani kwa baba yake mzazi, tangu awe rais mwaka 2008.
Msemaji wa White House amesema shabaha ya ziara hiyo, licha ya kuhudhuria mkutano, ni pamoja na kuongeza nguvu "ukuaji uchumi, kuongeza nguvu demokrasia na kuboresha usalama," barani Afrika.
Mkutano huo wa ujasiriamali ni tukio la kila mwaka tangu 2009 na unajumuisha wajasiriamali, wawekezaji, serikali na makundi mengine kwa nia ya kuboresha hali ya maisha duniani.
Safari hiyo pia itakuwa ya nne kwa rais Obama barani Afrika wakati wa urais waker, lakini hakuwahi kufika Kenya katika ziara zake za nyuma.