Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 05:54

Obama, Castro wakutana ana kwa ana


Rais Barack Obama na Rais Raul Castro wa Cuba wakipeanza mikono mjini Panama City, April 11, 2015.
Rais Barack Obama na Rais Raul Castro wa Cuba wakipeanza mikono mjini Panama City, April 11, 2015.

PANAMA CITY - Baada ya mkutano wa kihistoria na Rais Raul Castro wa Cuba, Rais Barack Obama wa Marekani amesema nchi hizo mbili "sasa ziko katika nafasi ya kusonga mbele kwa pamoja."

Viongozi hao wawili walikutana Jumamosi mchana kando ya mkutano wa viongozi wa mataifa ya America, muda mfupi baada ya wote wawili kuhutubia mkutano huo.

"Huu bila shaka ni mkutano wa kihistoria" baina ya Marekani na Cuba, alisema Obama akiashiria uhusama uliokuwepo baina ya nchi hizo. Baada ya miaka 50 ya sera ambayo haikufanya kazi "muda umefika kwetu kujaribu kitu kipya," alisema.

Rais Castro (katikati) na Obama wakipungia watu mikono
Rais Castro (katikati) na Obama wakipungia watu mikono

Hatua mpya itakuwa pamoja na kufungua balozi za nchi hizo katika miji ya Washington na Havana, alisema Rais Obama.

Obama alisema wakati wamarekani na wacuba wengi wamefurahiwa mabadiliko hayo ya sera, tofauti kubwa bado zingalipo baina ya nchi hizo. Aliongeza kuwa Marekani itaendelea kuzungumzia maswala ya demokrasia na haki za binadamu Cuba.

Viongozi hao wawili walikutana ana kwa ana muda mfupi baada ya kutoka hotuba zao mbele ya mkutano wa mataifa ya America. Mkutano huu ambao haukuwa rasmi ulikuwa wa kwanza baina ya viongozi hao tangu Rais Obama atangaze mwezi Disemba nia ya kurekebisha uhusiano wa Marekani na Cuba.

XS
SM
MD
LG