Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 15:46

Nigeria yatolewa nje ya michuano ya Afcon


Washabiki wa Tunisia wakishangilia katika mechi ya kombe la mataifa ya Afrika na Gambia Jan. 20, 2022.
Washabiki wa Tunisia wakishangilia katika mechi ya kombe la mataifa ya Afrika na Gambia Jan. 20, 2022.

Timu ya taifa ya Tunisia Carthage Eagles imefanikiwa kuwa timu ya pili kukata tiketi ya kuingia katika robo fainali ya michuano ya soka ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuibwaga Nigeria-Super Eagles kwa bao 1-0 katika uwanja wa Roumde Adjia mjini Garoua

Tunisia waliandika bao lao la kwanza na la ushindi kupitia kwa mchezaji Youssef Msakni anayechezea klabu ya Al Duhail ya Qatar katika dakika ya 47 ya mchezo.

Nigeria walijikuta wakicheza na mtu mmoja pungufu baada ya mchezaji wao mahiri Victor Iwobi kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Tunisia katika dakika ya 66 ya mchezo.

Kwa maana hiyo Tunisia sasa watakumbana na Burkina Faso katika robo fainali Jumamosi ijayo huko Garoua.

Matokeo haya yameshangaza baadhi ya mashabiki wa soka ukizingatia rekodi za timu hizi ambapo Nigeria waliingia katika hatua mtoano ya timu 16 kwa rekodi nzuri ya kushinda mechi zao zote katika kundi D na kuongoza kundi hilo wakati Tunisia waliingia baada ya kushika nafasi ya tatu katika kundi F na kupata nafasi katika timu 3 bora kuingia nafasi hiyo.

XS
SM
MD
LG