Ndege ya kwanza iliyobeba watoto wa Kipalestina waliojeruhiwa katika vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza imewasili katika Umoja wa Falme za Kiarabu leo Jumamosi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za misaada zilizoahidiwa na nchi hiyo kuwasaidia watoto 1,000.
Kundi hilo la watu 15 wakiwemo watoto na familia zao lilivuka Ukanda wa Gaza katika iivuo cha mpakani cha Rafah nchini Misri siku ya Ijumaa. Kisha wakasafiri kwa ndege kwenda Abu Dhabi, mji mkuu wa Imarati.
Watoto wadogo walikuwa wamelala kwenye mapaja ya mama zao wakati ndege hatimaye ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi. Baadhi ya viti vya ndege viliondolewa ili kutoa nafasi kwa watoto waliojeruhiwa sana ambao walihitajika kulala wakiwa wamejinyoosha.
Baadhi ya vijana hao walifungwa bandeji kwenye mikono na miguu. Wengine walikaa kimya karibu na wazazi au ndugu zao. Baadhi walisafiri peke yao. Hali ilikuwa ya utulivu na ukimya ndani ya ndege. Akina mama wengi walisema walikuwa wamechoka.
Forum