Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 07:06

Ndege za kivita za Russia zaripotiwa kuangushwa Ijumaa na Ukraine


Picha ya ndege za kivita sawa na zilizoagushwa na Ukraine
Picha ya ndege za kivita sawa na zilizoagushwa na Ukraine

Kwenye hotuba yake ya kila siku kwa taifa, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameshukuru marubani wa kijeshi waliotungua ndege mbili za kivita za Russia Ijumaa, kwenye mkoa wa Ukraine wa Kherson.

Wakati akitoa shukrani zake, Zelenskky alisema kwamba, “Ni vyema kila rubani wa Russia afahamu tutakachomfanyia kila muuwaji, hakuna atakayeachwa bila kuwajibishwa.” Hatima ya marubani wa ndege za Russia zilizoangushwa bado haijajulikana.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza kwenye taarifa yake ya kiintelijensia ya kila siku kuhusiana na vita vya Ukraine imesema kwamba vikosi vya Russia na Ukraine vinakabiliana na changamoto jipya kwenye uwanja wa vita, ambayo imetajwa kuwa” ongezeko lisilo la kawaida la panya kwenye uwanja wa mapigano.”

Inahofiwa kwamba panya hao huenda wakatafuta hifadhi kwenye magari ya kijeshi pamoja na ngome za kufanyia mashambulizi, suala ambalo huenda likawavunja moyo wanajeshi. Wizara hiyo imeongeza kusema kwamba panya hao huenda wakala nyaya za vifaa muhimu vya kijeshi, sawa na iliovyofanyika kwenye eneo hilo wakati wa vita vya pili vya dunia.

Ripoti ambazo hazijadhibitishwa zinasema kwamba tayari baadhi ya wanajeshi wa Russia wameanza kupata maradhi yanayoshukiwa kusababishwa na panya hao.

Forum

XS
SM
MD
LG