Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:15

Nchi zinazouza petroli duniani zapunguza uzalishaji kwa mapipa milioni 2 kwa siku


Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman Al-Saud na Katibu Mkuu wa OPEC Haitham al-Ghais wakipeana mikono kwenye makao makuu ya taasisi ya nchi zinazouza Petroli (OPEC) mjini Vienna, Austria Oktoba 5, 2022. REUTERS.
Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman Al-Saud na Katibu Mkuu wa OPEC Haitham al-Ghais wakipeana mikono kwenye makao makuu ya taasisi ya nchi zinazouza Petroli (OPEC) mjini Vienna, Austria Oktoba 5, 2022. REUTERS.

Jumuiya ya Nchi zinazouza petroli duniani, pamoja na Russia na wazalishaji wengine wa mafuta, Jumatano zilipunguza uzalishaji mafuta  kwa mapipa milioni 2 kwa siku.

Hatua ambayo inaweza kusaidia Moscow kulipia vita vyake vinavyoendelea na Ukraine na kuumiza nafasi ya Rais wa Marekani Joe Biden kupunguza zaidi bei ya mafuta ya petroli kwa madereva wa Amerika.

Kupunguzwa huko kwa uzalishaji kulionekana kama kemeo kwa Biden, ambaye alitembelea Saudi Arabia mnamo Julai katika kile ambacho sasa kimegeuka kuwa juhudi ya bure kumshawishi mzalishaji mkubwa wa pili wa mafuta duniani baada ya Marekani kukataa kupunguza uzalishaji.

Maafisa wa Ikulu ya Marekani walishambulia uamuzi wa Vienna wa nchi 23 ambazo ni za muungano wa OPEC+, ambao wachambuzi wanasema unaweza kuongeza hatari ya mdororo wa kiuchumi duniani katika miezi ijayo. Bei ya mafuta yasiyosafishwa imekuwa ikishuka kwa miezi kadhaa kwenye soko la dunia lakini imepanda katika siku za hivi karibuni kwa kutarajia kupunguzwa kwa uzalishaji wa OPEC

XS
SM
MD
LG