Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:19
VOA Direct Packages

Mwandishi wa habari wa Australia mwenye asili ya China aachiliwa kutoka jela ya China


Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese
Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese

Mwandishi wa habari wa Australia mwenye asili ya China ambaye  aliyehukumiwa kutokana na tuhuma za kijasusi na kushikiliwa nchini China kwa miaka 3 amerejea Australia, waziri mkuu wa taifa hilo Anthony Albanese amesema Jumatano.

Cheng Lei mwenye umri wa miaka 48 alikuwa mfanyakazi kwenye kitengo cha kimataifa katika shirika la utangazaji la serikali ya China la CCTV. Sasa hivi mwanadada huyo ameungana tena na watoto wake wawili mjini Melbourne, Albanese ameongeza kusema.

Kurejea kwake kumekuja kabla ya ziara iliyopangwa ya Albanese mjini Beijing mwaka huu ambayo tarehe yake bado haijatangazwa. Serikali ya Albanese imekuwa ikishinikiza kuachiliwa kwa Cheng pamoja na raia mwingine wa Australia mwenye asili ya China Yang Hengjun aliyeshikiliwa nchini humo tangu 2019.

Uhusiano kati ya China na Australia umeimarika tangu chama cha Albanese cha mrengo wa kati kushoto cha Labor kuchaguliwa baada ya miaka 9 ya utawala wa kikonsavative.

Forum

XS
SM
MD
LG