Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:04

Mwanamke atoa ushahidi katika kesi ya Ruto ICC


Naibu Rais wa Kenya, William Ruto akiwa ICC hukoThe Hague, September 10, 2013.
Naibu Rais wa Kenya, William Ruto akiwa ICC hukoThe Hague, September 10, 2013.
Shahidi wa kwanza katika kesi inayomkabili Naibu Rais wa Kenya William Ruto, alisimama Jumanne kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC- iliyoko huko The Hague kutoa ushahidi wake.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:56 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Shahidi huyo ambaye hakuonyeshwa sura yake kwa sababu za kiusalama anajulikana kwa namba 536 alikuwa ni mmoja kati ya walionusurika kwenye shambulizi la kuchoma moto lililotokea kwenye kanisa moja la Kiambaa huko Rift Valley baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Bwana Ruto anashtakiwa na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia ghasia za kikabila zilizotokea nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 1,000 na watu wengine 600,000 walilazimika kukimbia makazi yao na kwenda kuishi katika kambi za muda.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:11 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bwana Ruto anashtakiwa ICC akiwa na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang ambapo wote wawili wamekana kuhusika na mashtaka hayo.
XS
SM
MD
LG