Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:58

Mo Salah kucheza dhidi ya Uruguay


Kocha wa Misri Hector Cuper amesema kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji wake Mohamed Salah akacheza katika mchezo dhidi ya Uruguay, siku ya Ijumaa mjini Yekaterinbugh.

Mo Salah anayecheza Liverpool ya Uingereza aliumia katika mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kudodoshwa na mlinzi wa Real Madrid, Sergio Ramos.

Akiongea na wanahabari Alhamisi, kocha Cuper amesema Salah alifanya mazoezi na wenzake katika uwanja wa Yekaterinbugh, utapochezwa mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia.

Mshambuliaji Mo Salah wa Misri akiwa katika mazoezi ya mwisho Alhamisi, kabla ya kukabiliana na Uruguay, Ijumaa.
Mshambuliaji Mo Salah wa Misri akiwa katika mazoezi ya mwisho Alhamisi, kabla ya kukabiliana na Uruguay, Ijumaa.

Cuper amesema Salah anatarajiwa kucheza labda hitilafu zitokee dakika za mwisho, na itakuwa vigumu wao kusonga mbele katika kundi A bila ya kuwa na Salah. Kundi A lina timu za Russia, Saudi Arabia na Uruguay.

Wakati hayo yakiendelea, kocha wa Uruguay Oscar Tabarez, anaamini kwamba mshambuliaji wake Luis Suarez, sasa amekomaa kitabia toka alipofanya vibaya katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.

Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez akiwa katika mazoezi ya mwisho Alhamisi, kabla ya mchezo na Misri katika Kombe la Dunia Russia 2018, Ijumaa.
Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez akiwa katika mazoezi ya mwisho Alhamisi, kabla ya mchezo na Misri katika Kombe la Dunia Russia 2018, Ijumaa.

​Akiongea na wanahabari Alhamisi kuelekea mchezo wao na Misri, siku ya Ijumaa, amesema kwamba anajiamini kwamba Suarez amebadilika.

Suarez mwenye miaka 31 anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Uruguay katika kombe la dunia mwaka huu kutokana na uzoefu wake wa kucheza klabu ya Barcelona.

XS
SM
MD
LG