Mkataba huo uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki Julai mwaka jana, ulilenga kuzuia mzozo wa ukosefu wa chakula ulimwenguni kwa kuruhusu meli za chakula za Ukraine zilizozuiliwa na uvamizi wa Russia kuanza kupeleka chakula kwa njia salama kutoka kwenye bandari tatu za Ukraine.
Muda wa mkataba huo uliongezwa kwa siku 120 Novemba mwaka jana na hivyo muda wake utamalizika Machi 18. Muda wake utaongezwa iwapo hakutakuwa na upinzani, ingawa Moscow imeashiria kwamba itakubali tu iwapo masharti yaliyowekewa upelekaji wa bidhaa zake kwenye mataifa ya nje yataondolewa.