Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:45

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Libya awasilisha barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu  


Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Abdoulaye Bathily akizungumza wakati wa mkutano na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Waarabu katika mji mkuu wa Tripoli, Jumapili Januari 22, 2023.
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Abdoulaye Bathily akizungumza wakati wa mkutano na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Waarabu katika mji mkuu wa Tripoli, Jumapili Januari 22, 2023.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Libya alisema Jumanne aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akisema juhudi zake za upatanishi zimekabiliwa na upinzani wa ukaidi, na matarajio asiyotegemea na tofauti na maslahi ya watu wa Libya.

Abdoulaye Bathily aliteuliwa kushika wadhifa huo Septemba 2022. Haikuweza kufahamika mara moja ni lini alipanga kuachia ngazi.

Ninavyojua mimi nimefanya kadri niwezavyo, Bathily aliwaambia waandishi wa habari katika Umoja wa Mataifa mjini New York baada ya kutoa taarifa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Libya.

Libya imekuwa na amani na utulivu mdogo tangu uasi wa mwaka 2011 ulioungwa mkono na NATO, na iligawanyika mwaka 2014 kati ya mirengo ya mashariki huko Benghazi na maeneo ya magharibi huko Tripoli, huku tawala hasimu zikitawala katika kila mkoa.

Juhudi za kushawishi pande zinazopingana kufanya uchaguzi zimekuwa lengo kuu la diplomasia kwa miaka mingi, lakini kumekuwa na maendeleo madogo tangu usitishaji wa mapigano wa mwaka 2020 ambao ulisimamisha vita kubwa zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG