Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:33

Miss Kenya 2017 Magline Jeruto asema anataka kusaidia watoto wenye mtindio wa ubongo.


Miss Kenya 2017
Miss Kenya 2017

Mafanikio hayakufuati ila inabidi wewe uyafuate usingoje mtu akuletee fanya bidii katika kila jambo na usingioje kufanyiwa- Magline Jeruto

Miss Kenya 2017 Magline Jeruto aliingia katika tano bora ya michuano ya urembo duniani (Miss World) yaliyofanyika huko Sanya, China, Novemba 18, 2017.

Katika mahojiano yake na jukwaa la Vijana VOA amesema nia yake ni kusaidia watoto wenye mtindio wa ubongo katika jamii.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:06 0:00

Aidha ameongeza kwamba kilicho msukuma kufanya hivyo ni kuona kwamba watoto hao hawajapewa nafasi katika jamii.

Mwakilishi huyo wa Kenya amesema amejifunza mengi katika michuano hiyo akisema "si taji peke yake, unaangalia fursa kukutana na watu na kujifunza kutoka kwa wasichana wengine wa nchi nyingine duniani."

Na kuwataka Vijana wenzake wanaomtazama wawe wanamtegemea Mungu katika kila kitu na pia akiongeza "mafanikio hayakufuati ila inabidi wewe uyafuate, usingoje mtu akuletee fanya bidii katika kila jambo na usingoje kufanyiwa," mrembo huyo alisema.

XS
SM
MD
LG