Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:11
VOA Direct Packages

Milipuko yaripotiwa kwenye eneo la Morocco huko Sahara Magharibi


Bendera ya eneo la Sahara Magharibi ambalo pia linajulikana kama Sahrawi linalodhibitiwa na Morocco.
Bendera ya eneo la Sahara Magharibi ambalo pia linajulikana kama Sahrawi linalodhibitiwa na Morocco.

Milipuko minne Jumamosi jioni kwenye mji wa Smara kwenye  eneo linalodhibitiwa na Morocco la Sahara Magharibi  umeua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu kulingana na mamlaka za kieneo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taarifa iliyotolewa na mamlaka imesema kwamba milipuko hiyo iliharibu nyumba mbili, bila kutoa maelezo zaidi.

Morocco inachukulia Sahara Magharibi kuwa ni eneo lake, lakini kundi la Polisario Front linaloungwa mkono na Algeria linataka uhuru wa eneo hilo. Novemba mwaka 2020, Polisario Front lilisema limeanza tena mapigano, ingawa Umoja wa Mataifa ulisema kwamba hayakuwa yenye nguvu.

Morocco imesisitiza kwamba inachoweza kufanya ni kutoa uhuru wa kujitawala kwa eneo hilo na wala siyo uhuru kamili kama unavyodaiwa na Polisario na Algeria.

Forum

XS
SM
MD
LG