Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:23

Michel Aoun ameondoka kwenye makazi ya rais huko Lebanon


Rais wa Lebanon, Michel Aoun ambaye ameondoka madarakani, Oct. 13, 2022.
Rais wa Lebanon, Michel Aoun ambaye ameondoka madarakani, Oct. 13, 2022.

Bunge hadi sasa limeshindwa kukubaliana juu ya mrithi katika jukumu hilo, mwenye  uwezo wa kutia saini miswaada kuwa sheria, kuteua mawaziri wakuu wapya na kutoa ruhusa ya kuundwa  kwa serikali kabla ya kupigiwa kura na bunge

Michel Aoun rais mkristo mwenye umri wa miaka 89 ambaye aliiongoza nchi wakati wa matatizo ya kifedha na mlipuko mbaya kwenye bandari ya Beirut, aliondoka kwenye makazi ya rais Jumapili, na kuiacha nchi hiyo ikiwa haina kiongozi wa juu katika taifa lenye matatizo.

Bunge hadi sasa limeshindwa kukubaliana juu ya mrithi katika jukumu hilo, mwenye uwezo wa kutia saini miswaada kuwa sheria, kuteua mawaziri wakuu wapya na kutoa ruhusa ya kuundwa kwa serikali kabla ya kupigiwa kura na bunge.

Kama ilivyokuwa wakati wa zaidi ya nusu ya awamu ya Aoun madarakani, Lebanon kwa sasa inaongozwa na baraza la mawaziri la muda wakati waziri mkuu mteule amekuwa akijaribu kwa miezi sita kuunda Serikali.

Jumapili Aoun aliidhinisha kujiuzulu kwa serikali ya Najib Mikati, ambayo hata hivyo itabakia madarakani kama serikali ya muda, chanzo cha mahakama kimesema.

XS
SM
MD
LG