Waziri wa mambo ya nje wa Burundi ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuheshimu utaifa wa nchi yake kufuatia ukosoaji mkubwa dhidi ya uamuazi wa kuendelea na uchaguzi licha ya kuwepo ghasia.
Alain Aime Nyamitwe ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba haihitaji mtu yeyote , au nchi yoyote au kiongozi nje ya Burundi kufanya udiktekta dhidi ya burundi kuhusu mwelekeo inaotakiwa kuchukua.
Mji mkuu wa burundi Bujumbura umegubikwa na maandamano ya mara kwa mara tangu tangazo la mwezi April kwamba rais Pierre Nkurunzinza anataka kugombea tena muhula wa tatu wa uongozi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika julai 15.
Mahakama ya katiba iliamua kwamba rais nkurunzinza anaweza kugombea tena kwa sababu alichaguliwa na wabunge katika kipindi cha kwanza cha utawala wake.