Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:16

Mdahalo wa wagombea Makamu Rais Marekani wafanyika


Wagombea Makamu Rais wa Marekani, seneta Tim kaine (L) na gavana Mike Pence katika mdahalo huko Virginia.
Wagombea Makamu Rais wa Marekani, seneta Tim kaine (L) na gavana Mike Pence katika mdahalo huko Virginia.

Mdahalo wa kwanza na wa mwisho wa wagombea makamu rais nchini Marekani ulifanyika Jumanne usiku ambapo mdemocrat seneta Tim Kaine wa Virginia na mrepublican gavana Mike Pence wa Indiana walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza.

Mdahalo huo uliofanyika katika chuo kikuu cha Longwood huko Farmville katika jimbo la Virginia uliongozwa na mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha CBS, Elaine Quijano.

Seneta Tim Kaine akijieleza katika mdahalo
Seneta Tim Kaine akijieleza katika mdahalo

Seneta Kaine ndiye aliyeanza kufungua mdahalo kwa kujibu swali lililomtaka kueleza kwa nini anawania nafasi ya Makamu Rais ambapo alianza kwa kuelezea uzoefu alionao kama mwanasiasa ambaye amehudumu kuanzia ngazi ya halmashauri ya mji, meya, gavana na pia sasa ni seneta wa jimbo la Virginia, Marekani. Swali hilo hilo pia liliulizwa kwa gavana Pence ambaye alilijibu kwa kuelezea uzoefu wake wa muda mrefu akiwa amekulia katika mji mdogo huko Indiana na hatimaye amekuwa gavana katika jimbo hilo hilo la Indiana.

Gavana Mike Pence akijieleza katika mdahalo
Gavana Mike Pence akijieleza katika mdahalo

Mdahalo huo ulikuwa ukioneshwa moja kwa moja katika vituo mbali mbali vya habari Marekani. Mdahalo huu ni mfululizo wa midahalo mitatu ya wagombea nafasi za juu za uongozi katika White House kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani unaotarajiwa kufanyika Novemba nane.

Mdahalo wa pili wa wagombea urais Marekani unatarajiwa kufanyika Jumapili ya Oktoba tisa huko St.Louis katika jimbo la Missouri.

XS
SM
MD
LG