Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:59

Mazoezi ya kijeshi ya China karibu na Taiwan yawafanya washirika wake kukitembelea kisiwa hicho

Seneta wa Marekani Marsha Blackburn alipokutana na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen mjini Taipei, Taiwan. August 26, 2022. REUTERS.
Seneta wa Marekani Marsha Blackburn alipokutana na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen mjini Taipei, Taiwan. August 26, 2022. REUTERS.

Mazoezi makubwa ya kijeshi ya China karibu na Taiwan yamewafanya washirika wake kutembelea kisiwa hicho na kuonyesha mshikamano, amesema waziri wa mambo ya nje wa Taipei Joseph Wu ljumaa.

Mazoezi makubwa ya kijeshi ya China karibu na Taiwan yamewafanya washirika wake kutembelea kisiwa hicho na kuonyesha mshikamano, amesema waziri wa mambo ya nje wa Taipei Joseph Wu ljumaa.

Beijing inafanya mazoezi ya kijeshi ya anga ambayo hayajawahi kushuhudiwa ikiwa ni kutishia baada ya ziara ya Taiwan ya spika wa baraza la wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, aliyoifanya mwezi uliopita na kuzusha wasiwasi wa kiwango cha juu.

Wanasiasa wa Marekani wameshafanya ziara tatu baada ya ile ya Spika Pelosi, na ya hivi karibuni ikiwa ni ya seneta wa Tennessee, Marsha Blackburn, ambaye alikutana na rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen siku ya Ijumaa.

Taiwan imekuwa ikabiliwa na tishio la mara kwa mara la kuvamiwa na China, baada ya kujitangazia kujitawala yenyewe licha ya China kudai ni himaya yake na kutishia kuchukua kwa nguvu siku moja kama iikihitajika kufanyika hivyo.

XS
SM
MD
LG