Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 04:36

Mawasiliano na biashara zaendelea kuathirika tangu kufungwa kwa mitandao ya kijamii, Ethiopia


Picha ya mtu akitazama ukurasa wa mtandao wa kijamii kwenye simu yake.
Picha ya mtu akitazama ukurasa wa mtandao wa kijamii kwenye simu yake.

Miezi kadhaa baada ya Ethiopia kuweka marufuku kwenye mitandao ya kijamii, biashara za mawasiliano pamoja na makundi ya kutetea haki za kiraia zimeathirika pakubwa wakati kukiwa na changamoto ya kufikia wateja wao au kudhibitisha taarifa.

Machi mwaka huu serikali ilifunga mitandao ya Facebook, TikTok, Telegram na YouTube, kote nchini kufuatia kutoelewana na kanisa la ki Orthodox chini, ambalo baadhi ya viongozi wake walikuwa wanaitisha maandamano. Hata hivyo baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kama vile Amnesty International yamesema kwamba marufuku hiyo inahujumu haki ya kujieleza, na ni kunyume cha katiba ya Ethiopia, sheria pamoja na mikataba ya kimataifa.

Kupitia taaarifa naibu mratibu wa Amnesty mashariki na kusini mwa Afrika Flavia Mwangonya ameongeza kwamba hatua hiyo inaweka doa kwenye rekodi yenye mashaka ya uhuru wa vyombo vya habari nchini humo. Licha ya kwamba baadhi ya watu wanaweza kutumia mitandao ya kibinasfi ya VPN, bado ni vigumu kufikia wafuasi au wateja wao ndani ya nchi.

Forum

XS
SM
MD
LG