Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:43

Matumizi ya kijeshi duniani yaliongezeka kwa mwaka wa nane mfululizo


Mfano wa vifaa vya kijeshi vinavyotumika duniani
Mfano wa vifaa vya kijeshi vinavyotumika duniani

Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm matumizi ya kimataifa yaliongezeka kwa asilimia 3.7 kwa hali halisi, lakini matumizi ya kijeshi barani Ulaya yaliongezeka kwa asilimia 13 ongezeko lake kubwa zaidi la mwaka hadi mwaka katika angalau miaka 30.

Matumizi ya kijeshi duniani yaliongezeka kwa mwaka wa nane mfululizo hapo mwaka 2022 hadi kiwango cha juu cha dola trilioni 2.24 na ongezeko kubwa barani Ulaya hasa kutokana na matumizi ya Russia na Ukraine taasisi ya tanki la fikra la Sweden lilisema Jumatatu.

Matumizi ya kimataifa yaliongezeka kwa asilimia 3.7 kwa hali halisi, lakini matumizi ya kijeshi barani Ulaya yaliongezeka kwa asilimia 13 ongezeko lake kubwa zaidi la mwaka hadi mwaka katika angalau miaka 30 Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm-Stockholm International Peace Research Institute (SIPRI) ilisema katika ripoti.

Msaada wa kijeshi kwa Ukraine na wasiwasi juu ya tishio kubwa kutoka kwa Russia uliathiri sana maamuzi mengi ya matumizi ya mataifa mengine. Shirika huru la uangalizi la Sweden limesema kwamba kwa mwaka jana matumizi makubwa matatu ya silaha ni Marekani, China na Russia, ambazo kati yao zilichangia asilimia 56 ya matumizi ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG