Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:34

Matokeo zaidi ya uchaguzi Tanzania yaendelea kutolewa


Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi Tanzania

Tume ya uchaguzi Tanzania iliendelea kutoa matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili nchini humo. Tume hiyo ilimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge huko Mbeya mjini katika mkoa wa Mbeya ni mgombea wa chama cha upinzani cha CHADEMA, bwana Joseph Mbilinyi aliyetetea jimbo lake kwa kupata kura 97,675.

Baadhi ya matokeo yatangazwa
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:50 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mpinzani wake mkuu kutoka Chama cha Mapinduzi-CCM bwana Mwaliygo Shitambala alipata kura 46,894. Tume ya uchaguzi ilisema itaendelea kutoa matokeo rasmi kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa wiki nchini humo.

Watanzania wakisubiri matokeo ya October 25, 2015.
Watanzania wakisubiri matokeo ya October 25, 2015.

Hali ya usalama mkoani Mbeya ilielezewa na mwandishi wa sauti ya Amerika kuwa ni shwari licha ya kuwepo ghasia ndogo za hapa na pale zilizoongozwa na vijana wanaofurahia ushindi katika mitaa kadhaa ya mji huo. Polisi waliendelea kuimarisha usalama.

Wakati huo huo matokeo ya kiti cha ubunge mkoani Mwanza yalitangazwa. Mshindi katika jimbo la Ilemela lililokuwa na ushindani mkali dhidi ya chama tawala cha CCM na muungano wa baadhi ya vyama vya upinzani-UKAWA. Ilitangazwa kwamba jimbo la Ilemela lilichukuliwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi-CCM, bibi Anjelina Mabula aliyemshinda mpinzani wake bwana Kiwiya. Hata hivyo jimbo la Nyamagana bado linaendelea kuhesabu kura ambapo washindani wakuu ni Sanfrausi Mabula wa Chama cha Mapinduzi na bwana Ezekiel Wenje wa CHADEMA.

Miaka mitano iliyopita majimbo hayo mawili yalikuwa yakishikiliwa na chama cha upinzani cha CHADEMA.

XS
SM
MD
LG