Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:38

Mataifa ya kigeni yameagiza raia wake kuondoka Sudan huku vifo vikiongezeka


Jengo la makaazi mjini Khartoum limeharibiwa na mapigano yanayoendelea nchini Sudan. April 20, 2023.
Jengo la makaazi mjini Khartoum limeharibiwa na mapigano yanayoendelea nchini Sudan. April 20, 2023.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti jeshi la Sudan limesema Jumamosi linaratibu juhudi za kuwahamisha wanadiplomasia kutoka Marekani, Uingereza, China na Ufaransa kwa ndege za kijeshi wakati mapigano yakiendelea katika mji mkuu ikijumuisha pia katika uwanja mkuu wa ndege

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani hakuweza kuthibitisha ripoti kwamba jeshi la Sudan limekubali kusaidia kuwaondoa raia wa Marekani na wa mataifa mengine kutoka mji mkuu wa Sudan, Khartoum, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani aliiambia VOA mapema Jumamosi. Tunaendelea kuwasiliana kwa karibu na ubalozi wetu mjini Khartoum na kuwa na uwajibikaji kamili wa wafanyakazi wetu. Kwa usalama wao, siwezi kuzungumzia maelezo zaidi ya harakati zao au mahali walipo, alisema msemaji huyo.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti jeshi la Sudan limesema jumamosi kuwa linaratibu juhudi za kuwahamisha wanadiplomasia kutoka Marekani, Uingereza, China na Ufaransa kwa ndege za kijeshi, wakati mapigano yakiendelea katika mji mkuu, ikijumuisha pia katika uwanja mkuu wa ndege.

Jeshi la Sudan limesema mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amezungumza na viongozi wa nchi mbalimbali wakiomba kuondolewa kwa usalama raia wao na wanadiplomasia kutoka Sudan, nchi ambayo inashuhudia mapigano ya umwagaji damu kwa zaidi ya wiki moja iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 400.

Huku uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa nchini Sudan umefungwa, mataifa ya kigeni yameagiza raia wake kuchukua hifadhi hadi pale mipango ya kuwahamisha watu itakapofanyika.

XS
SM
MD
LG