Maseneta wa Republican na Democrat nchini Marekani wanaunga mkono ziara ya waziri wa mambo ya nje Marekani, Antony Blinken nchini China kuanzia Ijumaa lakini bado wana mashaka, iwapo hatua hiyo itasababisha mafanikio katika uhusiano na Beijing.
Blinken anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa kudumisha mawasiliano ya wazi kati ya nchi hizo mbili na kujadili masuala ya usalama wa kikanda, mabadiliko ya hali ya hewa, na uchumi wa dunia. Maafisa wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, pia wamesema suala la usafirishaji haramu wa dawa za kulevya aina ya Fentanyl kuja Marekani litakuwa sehemu muhimu ya mazungumzo hayo.
Kabla ya ziara hiyo, kitengo kinachohusika na masuala ya China katika VOA kilizungumza na maseneta kadhaa wa Marekani kuhusu matarajio yao ya mazungumzo hayo, ikijumuisha kama Blinken anapaswa kuelezea suala la kituo cha ujasusi cha China nchini Cuba, ambacho kilithibitishwa katika siku za hivi karibuni na maafisa wa Marekani.
Forum