Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:58

Martin Griffiths anaitembelea Sudan ambayo inashuhudia mapigano


Martin Griffiths, afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya kibinadamu. Sept. 28, 2021.
Martin Griffiths, afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya kibinadamu. Sept. 28, 2021.

Ghasia mbaya zilizosababisha vifo zilizuka Aprili 15 kati ya kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan, na naibu wake ambaye aligeuka kuwa mpinzani Mohamed Hamdan Daglo, anayesimamia vikosi vya Rapid Support Forces (RSF)

Mapigano yanayoendelea kati ya majenerali hasimu wa Sudan yamedhoofisha juhudi za kusitisha mapigano leo Jumatano wakati afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa alipowasili kwa mazungumzo juu ya namna ya kutoa misaada kwa mamilioni ya raia waliokwama.

Ziara ya afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths imekuja siku moja baada ya nchi jirani ya Sudan Kusini kutangaza kuwa pande zinazohasimiana zimekubaliana kwa pamoja kusitisha mapigano kwa siku saba.

Ghasia mbaya zilizosababisha vifo zilizuka Aprili 15 kati ya kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan, na naibu wake ambaye aligeuka kuwa mpinzani Mohamed Hamdan Daglo, anayesimamia vikosi vya Rapid Support Forces (RSF).

Takriban watu 550 wameuawa na wengine 4,926 kujeruhiwa kulingana na takwimu za hivi karibuni za wizara ya afya ya Sudan siku ya Jumatano takwimu ambazo huenda hazijakamilika.

XS
SM
MD
LG