Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:47

Marekani yamtafuta Protais Mpiranya kwa kushiriki mauaji ya halaiki 1994


Ramani ya Rwanda
Ramani ya Rwanda

Protais Mpiranya, kamanda wa zamani wa Presidential Guard of the Rwandan Army, anatafutwa kwa kushiriki katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda. 

Mwezi April mwaka 1994, wakati ghasia za wenye msimamo mkali sana nchini Rwanda walipoanzisha kampeni ya umwagaji damu ya kusafisha kabila moja, Mpiranya aliongoza kikosi maalum cha Rais. Anashutumiwa kwa kuwa na jukumu kubwa katika kupanga mauaji ya halaiki, ikiwemo kutoa mafunzo kwa makundi ya kijeshi na kugawa silaha. The Presidential Guard of the Rwandan Army, chini ya uongozi wa Mpiranya, kinashutumiwa kumuuwa waziri mkuu wa wakati huo Agathe Uwilingiyimana, na walinda amani kumi wa Ubelgiji ambao walikuwa walinzi wake. Wakati wote wa mauaji ya halaiki, kikosi maalum cha ulinzi cha rais kiliripotiwa kuwa kikosi kikuu kilichoendesha ukiukaji wa sharia na uharibifu.

Kwa hili na uhalifu mwingine, mahakama ya kimataifa inayohusika na uhalifu wa Rwanda-ICTR, hivi sasa inajulikana kama International Residual Mechanism for Criminal Tribunals, ilimfungulia mashtaka Mpiranya kwa mashtaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu wa vita na ilitoa waranti ya kukamatwa kwake.

Marekani inashirikiana na serikali nyingine, Umoja wa Mataifa na Residual Machanism, kufanya iwe vigumu kwa Mpiranya na wenzake wanaotafutwa kwa mauaji kuendelea kukwepa sharia. Kufanikisha suala hili, Marekani inatoa zawadi ya hadi dola milioni tano kwa taarifa zinazopelekea kukamatwa kwake.

Kama wewe au mtu yeyote unayemfahamu ana taarifa juu ya harakati na mahali alipo Proitasi Mpiranya, unaweza kutoa ripoti kwa usiri mkubwa. Tafadhali nenda kwenye ubalozi wa Marekani uliopo karibu na wewe au tovuti ya ubalozi mdogo kuwasiliana na ofisi ya usalama katika eneo, andika barua pepe U.S, War Crimes Rewards Program at WCRP@state.gov, au wasiliana nasi kupitia WhatsApp kwenye +1=202-975-5468. Unaweza pia kutembelea ukurasa wetu wa Facebook at www.facebook.com/war-crimes-rewards-program (www.facebook.com/war crimesrewards program) au tufuatilie kwenye Twitter at www.teitter.com/WarCrimesReward(www.twitter.com/war crimes reward) kwa picha za watoro wanaotafutwa.

Ripoti zote zinazoaminika zitachunguzwa na wajihi wa watoaji wote wa taarifa utawekwa siri.

XS
SM
MD
LG