Marekani na Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano ya muda mrefu katika mzozo wao wa siku nyingi juu ya ruzuku za ndege.
Washington inasimamisha kwa miaka mitano ushuru kwa nchi za Ulaya ambayo iliidhinishwa na Shirika la Biashara Ulimwenguni kwa ruzuku isiyo ya haki kwa shirika la Airbus, ambayo ndio mtengenezaji mkubwa wa ndege na mshindani mkuu wa Boeing ya Marekani.
"Mkutano huu umeanza kwa mafanikio", alisema Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen mwanzoni mwa mazungumzo rasmi Jumanne na Rais wa Marekani Joe Biden. "Kwa kweli hii inafungua ukurasa mpya katika uhusiano wetu kwa sababu tunahama kutoka kwenye madai hadi ushirikiano kwenye ndege baada ya miaka 17 ya mzozo.
Makubaliano hayo yanasuluhisha kikwazo cha muda mrefu katika uhusiano wa kibashara kati ya Marekani na Ulaya. Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Katherine Tai aliwaambia waandishi wa habari juu ya wito wa mkutano.
Badala ya kupigana na mmoja wa washirika wetu wa karibu, mwishowe tunakutana pamoja dhidi ya tishio la pamoja. Tulikubaliana kufanya kazi pamoja ili kupinga na kukabiliana na vitendo vya China visivyo vya soko katika sekta hii kwa njia maalum zinazoonyesha viwango vyetu vya ushindani wa haki.