Hatua hiyo mpya inafikisha jumla ya vituo 9 vya kijeshi vinavyoweza kutumiwa na jeshi la Marekani nchini humo, na imekuja wakati waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alipokutana na wakuu wa kijeshi pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama wa taifa.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa leo haikutaja vilipo vituo hivyo , lakini imeongeza kusema kwamba vitasaidia kwenye majanga ya kibinadamu na yale yanatokana na hali ya hewa nchini Ufilipino, miongomi mwa changamoto nyingine.
Ziara za ya Austin imekuja baada ya miezi kadhaa ya mashauriano kati ya Marekani na Ufilipino kwa lengo la kurejesha uhusiano pamoja na kukabiliana na tishio la China na hasa kwenye bahari ya South China Sea.