Muongoza mashitaka huyo atakuwa mjini The Hague, Uholanzi, kwenye ofisi ya Idara ya ushirikiano wa haki za Uhalifu ya EU maarufu Eurojust. Garland ameyasema hayo baada ya kufanya kikao na muongoza mashitaka wa Ukraine Jenerali Andriy Koatin.
Ameongeza kusema kwamba mshauri maalum wa Marekani atatumwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kyiv katika msimu wa joto unaoanza sasa. Amesema kwamba waongoza mashitaka wa Ukraine wamekuwa wakishirikiana na wizara ya sheria ya Marekani katika kuchunguza ukatili wa kivita, ambapo Marekani ina uwezo wa kuwawajibisha wale wanaojeruhi au kuuwa wamarekani.
Bunge la Marekani hivi karibuni liliongeza mamlaka ya wizara hiyo ya kuweza kuwafungulia mashtaka wahalifu wa kivita wanaopatikana ndani ya Marekani.