Marekani inazidi kupungukiwa na fedha na wakati kuisaidia Ukraine katika kukabiliana na uvamizi wa Russia, mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi na bajeti Shalanda Young, alionya katika barua aliyomwandikia spika wa bunge Mrepublikan Mike Johnson, na viongozi wengine wa bunge.
Young amesema katika barua hiyo kwamba kufikia mwisho wa mwaka huu, Marekani haitakuwa tena na fedha za kutuma silaha na msaada kwa Ukraine. “Haitaweza kuendelea kupigana,” Young amesema kuhusu Ukraine, akielezea kuwa Marekani tayari imeishiwa pesa za kuendeleza uchumi wa Ukraine.
Mwezi Oktoba, utawala wa Biden uliliomba bunge karibu dola bilioni 106 kufadhili mipango madhubuti ya Ukraine, Israeli na usalama wa mipaka ya Marekani. Ufadhili kwa Ukraine umekuwa na utata wa kisiasa huku baadhi ya wabunge wanaoegemea mrengo wa kulia katika bunge linalodhibitiwa na kidogo cha chama cha Republikan.
Forum