Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 22:47

Marekani kupunguza utoaji gesi chafu


Rais Barack Obama.
Rais Barack Obama.

Ikulu ya Marekani - White House - Jumanne ilitoa pendekezo la Rais Barack Obama la kupunguza utoaji wa gesi chafu nchini Marekani hadi asilimia ishirini na nane,chini ya kiwango cha mwaka 2005 katika kipindi cha muongo mmoja kama sehemu ya mkataba wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Pendekezo hilo linahusisha sera nyingi ambazo tayari zinafanyiwa kazi kama vile matumizi ya magari yasiyotumia mafuta mengi, kupunguza matumizi ya nishati kwenye majengo na vifaa pamoja na program ya kuondoa gesi ya HFC itokayo kwenye friji. Kwenye taarifa iliyotolewa kwenye mitandao, White House iliashiria sheria mpya zitakazopunguza moshi kutoka kwa wachimba mafuta na gesi ya Carbon kutoka kwa viwanda.

Mpango huu unafuatia ahadi ya Bw Obama ya mwezi Novemba mwaka jana mjini Beijing ya kupunguza kiwango cha gesi chafu kwa asilimia ishirini na sita hadi ishirini na nane. Haya yamejiri kabla ya mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kufanyika mjini Paris Ufaransa baadaye mwaka huu.

XS
SM
MD
LG