Mapigano yaliendelea Ijumaa huko Gaza huku maafisa wa afya katika eneo hilo wakiripoti watu 105 waliuawa usiku kucha kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. Shirika hilo la habari limeinukuu ofisi ya habari ya Hamas ikisema mashambulizi ya anga na makombora ya Israel yalilenga mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis.
Wakati huo huo shirika la habari la Reuters limeripoti Ijumaa kwamba vikosi vya Israel vilishambulia viunga vya Rafah kusini mwa Gaza ambako maelfu ya watu wamekimbilia tangu Israel ilipoanza mashambulizi yake dhidi ya Khan Younis, moja ya mashambulizi makubwa sana tangu vita hivyo vilipoanza.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva Ijumaa, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), Jens Laerke alielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuongezeka kwa uhasama huko Khan Younis na ongezeko la idadi ya watu wanaokimbia kwenda Rafah.
Forum