Wadau wa ndondi nchini Kenya waliandaa pambano la maonyesho ya kumuenzi Raphael Shigali mwenye umri wa miaka 35, ambaye alikuwa bingwa wa uzani wa Bantam katika mji mkuu Nairobi.
Shangwe na furaha zilisikika wakati mabondia wa Kenya katika mtaa wa Eastlands jijini Nairobi waliposhuka ulingoni lakini pia maumivu ya kihisia na hasira.
Mchezo huu wa maonyesho ulifanyika kwa heshima ya bondia Raphael Shigali.
Kocha Raphael Shigali, ambaye vyombo vya habari vya Kenya viliripoti aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga kodi ya Julai 12 kwenye mtaa aliokulia.
Eneo liitwalo Jericho na shirikisho la ndondi la nchini humo wanachangisha fedha kumzika Shigali ambaye alikuwa bingwa wa uzani wa Bantam mjini Nairobi.
Moses Shillisia ni kocha wa ndondi wa Nairobi anasema Raphael alikuwa mtu mzuri na mwenye kupendwa na kila mtu.
Akiwa ameolewa na Shigali kwa miaka 13, Judy Wanjiku amebaki peke yake kuwatunza watoto wao watatu.
Anasema mume wake hakushiriki maandamano lakini alikuwa akitembea tu nyumbani na kufanya shughuli zake.
Shigali alisifiwa na wengi kwa kusaidia kutangaza ndondi katika jamii yake.
Wanjiku anasema anataka zaidi ya medali zake kumkumbuka.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linasema takriban watu 18 wameuawa mwezi huu katika mapambano na polisi wakati wa maandamano yaliyoongozwa na upinzani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha na kupandishwa kodi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanawalaumu polisi wa Kenya kwa kuwa wepesi kutumia risasi za moto wakati wa maandamano na wametaka uchunguzi ufanyike haraka kuhusu vifo hivyo.
Msemaji wa polisi wa Kenya alikataa kuzungumzia mauaji hayo ikiwa ni pamoja na ya Shigaliisipokuwa kwa kusema kuwa suala hilo linachunguzwa.
Lakini pamoja na mashtaka machache ya polisi wa Kenya, uwezekano ni mdogo kwa mjane wa Shigali kuona haki inatendeka.
kwa vile serikali na upinzani kufikia sasa hawataki kurudi nyuma, watoto wa Wanjiku wana uwezekano wa kuwa sio wa mwisho kuachwa bila baba.
Forum