Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 00:56

Mali yaahidiwa msaada wa zaidi ya dola bilioni 4


Wajumbe katika mkutano wa wafadhili wa Mali mjini Brussels, Mei 15, 2013.
Wajumbe katika mkutano wa wafadhili wa Mali mjini Brussels, Mei 15, 2013.

Serikali ya Mali ilitumai kuwa wafadhili wa kimataifa watakuwa wakarimu kwa taifa hilo la Afrika magharibi, na hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Wafadhili wa kimataifa wameahidi zaidi ya dola bilion 4 kama msaada wa amani na maendeleo nchini Mali. Kiasi hicho cha fedha kimepita matarajio ya awali katika mkutano uliofanywa Jumatano mjini Brussels.

Serikali ya Mali ilitumai kuwa wafadhili wa kimataifa watakuwa wakarimu kwa taifa hilo la Afrika magharibi, na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kiasi cha fedha zilizoahidiwa katika mkutano huo zilikuwa takriban dola bilion 4.2, hiyo ikiwa bilion moja zaidi kuliko serikali ya Mali ilivyotarajia.

Katika mkutano na waandishi habari mjini Brussels, Francois Hollande, rais wa Ufaransa, ambaye ni miongioni mwa walioandaa mkutano huo pamoja na umoja wa ulaya, alisema mkutano huo ulikuwa wa ufanisi mkubwa.

Rais wa Mali Diacounde Traore anasema kando na fedha, mkutano wa Brussels umejadili pia juhudi za pamoja za kukabiliana na ugaidi na makundi ya waislam wenye siasa kali za ambao si kitisho tu kwa Mali lakini pia kwa jumuiya ya kimataifa.

Mali ilikumbwa na mzozo mwaka jana kufuatia mapinduzi yaliyowafanya wanamgambo wa kiislamu kudhibiti sehemu kubwa za kaskazini mwa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG